MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Dodoma, imewakuta na kesi ya kujibu washtakiwa wanne wa kesi ya kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume na maumbile binti mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam.
Washtakiwa hao wamekutwa na kesi ya kujibu jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Zabibu Mpangule na watatakiwa kujitetea kuanzia kesho.
Upande wa Jamhuri ulileta jumla ya vielelezo 12 na mashahidi 18 ambao walitoa ushahidi kuhusu kesi inayowakabili washtakiwa hao ambao ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Clinton Damas, maarufu Nyundo, askari Magereza, Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama jana, wakili wa washtakiwa hao, Godfrey Wasonga, alisema mahakama imetoa uamuzi kuwa washtakiwa wote wana kesi ya kujibu na wanatakiwa kujitetea kuanzia kesho na wao wameshajipanga.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED