Fowadi 6 wanaoweza kumrithi Jesus Arsenal

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:18 AM Jan 20 2025
Alexander Isak.
Picha: Mtandao
Alexander Isak.

ARSENAL imejikuta katikati ya dirisha la usajili la Januari huku eneo moja la kikosi chao likihitaji kuongezewa nguvu.

Kutokana na majeraha ya muda mrefu ya Bukayo Saka na Gabriel Jesus, ambaye aliumia misuli ya nyama za paja katika kichapo cha wikiendi moja iliyopita kutoka kwa Manchester United kwenye Kombe la FA, Arsenal italazimika kufikiria kuimarisha safu yao ya ushambuliaji wakati wa dirisha la majira haya ya baridi.

'Washikabunduki' hao wamekuwa na wakati mgumu wa usajili kwa kushindwa kumsajili mshambuliaji wa kati, na licha ya uwapo wa Kai Havertz, lakini bado kunaonekana kunahitaji la kumnunua mshambuliaji namba tisa. 

Kutumia fedha sasa ni jambo la lazima baada ya majeraha ya muda mrefu.

Hawa hapa ni washambuliaji sita ambao Arsenal wanaweza kujaribu kuwanunua Januari hii. 

Alexander Isak

Hakuna siri kuhusiana na Arsenal kutaka kumnunua mshambuliaji wa Newcastle United, Alexander Isak. Nyota huyo wa Sweden, ambaye amefananishwa na gwiji wa Washikabunduki hao, Thierry Henry, kwa muda mrefu amekuwa akipendekezwa kuhamia London Kaskazini, na kiwango chake cha kuvutia cha msimu huu wa 2024/25 kimeongeza mijadala kuhusu mustakabali wake.

Isak ametengeneza mabao 15 na asisti nne katika mechi 22 alizochezea 'Magpies' msimu huu huku akionekana kuongeza idadi yake ya mabao 27 pamoja kutoka msimu uliopita. Mshambuliaji huyo mwenye nguvu na kasi amefunga katika mechi zote mbili dhidi ya Arsenal msimu huu.

Kumsajili Isak hakutakuwa jambo rahisi. Newcastle inaripotiwa kuwa inamthaminisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, kwa pauni milioni 150, ada ambayo itawakatisha tamaa wengi Ulaya. Januari inaweza kuonekana mapema sana kwa mabadiliko kama hayo, haswa na Arsenal katika nafasi dhaifu ya mazungumzo. 

Viktor Gyokeres

Raia mwingine wa Sweden ambaye Arsenal imekuwa ikivutiwa naye kwa muda mrefu ni Viktor Gyokeres, ambaye mwenyewe amefanikiwa kuwa mmoja wa washambuliaji bora zaidi duniani tangu ahamie Sporting CP mwaka 2023. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Brighton & Hove Albion alifunga mabao 43 na kusaidia 14 kwenye mechi 50 alizocheza katika kampeni ya kwanza huko Lisbon.

Gyokeres anastaili, inayofanana na Isak kuhusiana na kasi yake na umbile. Bei inaweza isiwe juu sana lakini bado itafanya macho miamba hao wa Kaskazini mwa London kuwa na wakati mgumu, kwani anakadiriwa kuwa na thamani ya takriban pauni milioni 70 hadi 90 zinazohitajika kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka kwa mabingwa watetezi wa Ureno.

Huku Gyokeres akiwa bado hajajaribiwa kwenye Ligi Kuu England, ana umbile na ukatili unaohitajika kwa kikosi chochote kwenye kuzifumania nyavu. Mabao matano katika mechi sita za Ligi ya Mabingwa Ulaya - ikiwa ni pamoja na hat-trick dhidi ya Manchester City - inathibitisha uwezo wake.

 Benjamin Sesko

Tamaa ya Arsenal ya kuimarisha safu ya ushambuliaji si jambo geni. Benjamin Sesko aliripotiwa kuwa mlengwa mkuu wa klabu hiyo mwanzoni mwa msimu wa majira ya joto uliopita, lakini haraka akasaini mkataba wa nyongeza na RB Leipzig ambao ulifanya uhamisho wa kwenda Ligi Kuu England kutowezekana.

Akiwa na umri wa miaka 21 pekee, mshambuliaji huyo wa Slovenia bado hajaamuru mechi kwa njia sawa na wenzake, lakini ametoa namba thabiti mapema katika kazi yake. Alifunga mabao 18 akiwa na Leipzig msimu uliopita, hesabu ya kuheshimika.

Arsenal watakuwa wanalipa uwezo na Sesko taayari ni mshambulizi mzuri, lakini ana uwezo wa kuibuka namba tisa anayekipiga katika timu ya Emirates. Ada yake inatajwa kuwa kati ya pauni milioni 50 hadi 70 na inaweza kuwa kikwazo kwa Arsenal Januari hii.

 Santiago Gimenez

Ikiwa Kocha Mikel Arteta anataka mapendekezo kuhusu Santiago Gimenez, anahitaji tu kumpigia simu Kocha wa Liverpool, Arne Slot. Mholanzi huyo alisaidia kumlea mshambuliaji huyo wa Feyenoord walipokuwa pamoja huko Rotterdam, akiwa na mabao 49 katika misimu yake miwili iliyopita.

Mshambuliaji huyo wa kati mrefu na mwenye uwezo mkubwa wa kufunga ana umri wa miaka 23 tu, mchezaji huyo wa Kimataifa wa Mexico ana muda mwingi wa kutatua matatizo yoyote.

Bila shaka, Ligi Kuu ya Uholanzi, Eredivisie, ina rekodi mchanganyiko linapokuja suala la kuzalisha vipaji vya kiwango cha Ligi Kuu England, lakini Arsenal wanaweza kutuzwa haraka ikiwa watacheza kamari kwa Gimenez. Mshambuliaji huyo karibu ajiunge na Nottingham Forest msimu wa majira ya joto na huenda akawa mbadala wa bei nafuu kwa wengine kwenye orodha ya wanaotamaniwa na Washikabunduki hao.

 Liam Delap

Baada ya muda wa mkopo wa tatu na viwango tofauti vya mafanikio, Liam Delap hatimaye alifanikiwa kuhamia Ipswich Town kutoka Man City wakati wa majira ya kiangazi. Walimnunua kwa kitita cha pauni milioni 20 na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, anaweza kuthibitisha mwokozi wao mwishoni mwa msimu.

Delap, mtoto wa mchezaji wa zamani wa Stoke City, Rory, ametengeneza mabao nane katika kipindi chake cha kwanza cha nusu msimu akiwa na Ipswich na amevutia macho kwa mbinu ya kushambulia. Ana uwezo mkubwa wa kuwapa wakati mgumu mabeki bora wa ligi.

Januari inaweza kuja mapema sana kwa Delap na Arsenal - ikiwa Washikabunduki hao wanavutiwa na kinda huyo, bila shaka - huku Ipswich ikiwa na uwezekano wa kuidhinisha kuondoka kwa hali yoyote. Bado, ni mmoja ambaye angeweka alama kwenye masanduku kadhaa kwa Washikabunduki. 

Jonathan David

Ni Robert Lewandowksi, Harry Kane na Erling Haaland pekee waliofunga mabao mengi katika ligi tano bora za Ulaya kuliko nyota wa Lille, Jonathan David mnamo 2024. Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Canada alifikisha mabao 36 katika mwaka wa kalenda, idadi sawa na Kylian Mbappe na saba zaidi ya Mohamed Salah na Cole Palmer.

Sababu pekee ambayo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anachukuliwa kuwa chaguo la 'gharama nafuu' Januari ni kutokana na ukweli kwamba mkataba wake unaisha msimu huu wa majira ya joto. Jambo kama hilo linaweza kuingia mikononi mwa Arsenal, huku Lille ikitarajiwa kukubali ofa ya takriban pauni milioni 20 hadi 25.

Ingawa Arsenal inaweza kusubiri na kumsajili David kwa msimu huu wa majira ya joto, kuweka fedha Januari itawaruhusu kushinda foleni na kuwapa mmoja wa washambuliaji wa kati bora zaidi Ulaya kwa kipindi cha pili cha msimu huku wakitarajia kumaliza ukame wao wa taji.