Mahmoud Ali Youssouf; Mwenyekiti mpya AUC, alivyojinadi, Dar mtaji wake, uliomvusha Ethiopia

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 08:30 AM Feb 21 2025
Mwandishi wa makala hii, Christina Mwakangale, akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa AUC, Januari 23, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mwandishi wa makala hii, Christina Mwakangale, akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa AUC, Januari 23, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

MAHAMOUD Ali Youssouf (59), ni mwanadiplomasia kwa takribani miaka 33 amekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Djibouti, kwa miaka isiyopungua 20.

Kwa sasa ndiye Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), akichukua nafasi ya Moussa Faki, aliyemaliza muda wake, baada ya uchaguzi  Jumamosi, Februari 15, 2025.

Youssouf, anataja dhamira yake kuiinua Afrika kiuchumi, kwa kuvifanya mifumo ya jumuiya kikanda kuwa hai, akisema msingi ni amani na usalama.

Anajimtambulisha kuwa na uzoefu katika masuala ya diplomasia pamoja kwa sura pana, akijinasibu kuwa miongoni mwa wenye sifa za kuiongoza.

Wakato akijinadi jijini Dar es Salaam anasema kwa kujiamini.

Mnamo Januari 23 mwaka huu, akiwa jijini Dar es Salaam na kukutana na waandishi wa habari, akaeleza viliko vikwazo kiuchumi barani na dhamira yake ya namna ya kuving’oa.

Dakika 30 zilimtosha kunadi hoja yake jijini Dar es Salaam, kabla ya kwenda kwenye kinayang’anyiro kufikia jukumu alilofanikiwa kulipata, sasa anaandaa safari mpya kuelekea Afrika inayotakiwa na wakazi wake, hadi ifikapo mwaka 2063 ukomo wake utakapofika.

Anataja changamoto za barani Afrika zilizodumu miaka mingi katika maeneo yote, kuanzia sekta ya afya, ulinzi na usalama, uchumi, kilimo, miundombinu na sasa kwenye mawasiliano. Fuatilia ufafanuzi wake kwa waandishi jijini Dar es Salaam:

AMANI, USALAMA, UTULIVU

“Tuna maeneo  mengi ambayo yana migogoro. Chombo cha Umoja wa Afrika (AU) na vingine kikanda kama ECOWAS (Umoja wa Nchi za Magharibi Afrika), SADC (Umoja Kuisini mwa Afrika), vinalenga kuleta amani na kulinda katika bara, ingawa kuna mgogoro DRC Mashariki kwa takribani miaka 25, hata Libya, Sudan, Sahel nako ni hivyo hivyo.

“Binafsi na tume yangu mpya, tutajikita kwenye masuala mawili, matatu hasa kuhusu amani na usalama.

“Kuna vyombo kadhaa vinavyoshughulikia, ila mtazamo wangu ni kuvifanya vifanye kazi ipasavyo. Hasa tutajikita kujikinga kabla ya migogoro kutokea.

JESHI  TAYARI, BARA JUMUISHI

“Afrika tuna kanda tano, inatakiwa kuwa na jeshi lililoko tayari inasubiri kazi. Hiyo ni kwa kila kanda na inapotokea dharura tunalituma na sukuma  kuwa na namna ya kuzuia, tutaleta tofauti.

“Tuna kaulimbiu kuhusu Afrika tuitakayo sisi AU, ili kuwa Afrika ya Maendeleo kibiashara. Kwa mfano, ‘Biashara Ndani ya Afrika,’ kwa sisi mataifa yetu tunasafirisha nje malighafi kwa asilimia 80, hatupati thamani mazao yetu na tunapoteza fedha.

‘Tunapaswa kubadilika ili kupata thamani ya mnyororo wa thamani katika mazao yetu. Mwaka 2063 tunataka tuwe na Afrika tuitakayo, inayotuhusu, kuvuka mipaka na kuondoa vikwazo.

“Mfano, Kuna vikwazo. Kuna sehemu tunakwama hasa kwenye miundombinu, hata safari za anga kuna wakati inakupasa utoke barani Afrika uende Ulaya ndio ufike nchi nyingine ya Afrika.

“Ndege zetu nyingi hazina safari za kufika nchi hadi nchi moja kwa moja. Tunapaswa kukiondoa kikwazo hiki, tuna mengi ya kufanya. 

BIASHARA, MIUNDOMBINU, SERA 

“Kuna vikwazo vya kibiashara kwa sababu kwenye mipaka yetu, tunahitaji kushughulikia vibali vingi na kwa muda mrefu. Tunahitaji kubadilika katika hili.

Miundombinu haiji kwa usiku mmoja, tunahitaji kuwekeza na kuwa na miundombinu imara, Dar es Salaamna miundombinu mizuri ndio inatakiwa hata kwenye mipaka yetu. Nimeona nikitoka airport (JNIA), 

“Tunaposema maendeleo ya kibiashara tunahitaji pia sera. Kwa mfano kuwa sera zinazoona ni muhimu, ili kuweka utulivu wa kibiashara. Hili tuliwahi kukubaliana Abuja miaka 30 iliyopita.”

VIJANA AFRIKA

” Katika kila wananchi wa kiafrika bilioni 1.4 miongoni mwao milioni 600 ni vijana. Kuna matarajio makubwa kwao vijana wanatarajia mengi kutoka kwa viongozi katika maamuzi pia

“Hapa, pia kuna lengo la jinsi, katika kuleta mabadiliko ya uongozi wahusishwe wote na vijana washiriki. Tutabadilika tuwalete vijana katika hili.”

MABADILIKO TABIANCHI

“Ni suala ambalo halijawakilishwa vizuri ingawa hivi karibuni kulikuwa na integrated kwenye G20 kwamba Afrika inahitaji kuwa na wajumbe wawili wa kudumu katika kura ya Veto na katika Bodi za Kimataifa.

AFYA NA INTANETI

“Tunataka tuwe na Afrika ambayo inajitegemea yenye viwanda vya dawa, tuwe na chanjo yetu na inapofika wakati wa janga tujitetegemee wenyewe.

“Hii inawezekana. Tayari tuna viwanda vikubwa Afrika Kusini na Senegal, tunaweza maeneo mengine pia.

“Kama hatuna usalama wa chakula, dawa, tunapaswa kuwa na ‘Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi’. Nitaweza! Nimekuwa katika masuala haya kwa muda mrefu, nalifahamu bara la Afrika.

“Kipaumbele cha kwanza ni kuwa na Intaneti inayoiunda Afrika Kidemokrasia. Nitahakikisha hili, kama tunataka kuondokana na changamoto eneo hilo inapaswa 

“Vijiji vya Afrika vina intaneti ya Bei rahisi na imara. Mfuko wa kidigitali ni muhimu ili vijana wajasiriamali wawe eneo hilo kufanya kazi, pesa inahitajika kwenye miradi hiyo

Kuwa na digitali ni maendeleo, yajayo, dunia inabadilika haraka tunahitaji kubadilika pia.

 KUJITEGEMEA KIUCHUMI 

“Tutazungumziaje uhuru eneo hili, wakati bado tunawategemea wadau kutusaidia masuala yetu ya kifedha?

“Bajeti ya AU mwaka 2025 ni takribani Dola milioni 600 na hapo hapo tunategemea Dola milioni 300 kutoka kwa wadau!

“Kilimo; nikiwa Kampala (Uganda) miaka michache iliyopita kwenye kongamano la eneo hilo, mikakati iliwekwa. Hapa nitajikita na maazimio yaliyotolewa. Kilimo ni eneo muhimu la kuwekeza 

“Kupitia umoja wetu waafrika tunaweza kuleta mustakabali ya nchi na bara letu. Hatujafikia hatua kuona jamii zetu zikifanya kazi pamoja, kipaumbele ni kufungua maeneo hayo kupitia miundombinu, usalama, amani, kisiasa.

“Kama tumeweza kuwa na vyombo vya Umoja kikanda, tunaweza pia kufanya kazi kwa umoja.

“Tunahitaji kuzibadili changamoto kuwa fursa, si kwa siku moja, lakini kwa uzoefu nilionao pamoja na tume.”