MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara, John Heche amesema yeye na Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu wanatarajia kupeleka ajenda ya no reform, no election hadi nje ya nchi.
Akizungumza na wanachama wa chama hicho wa Kanda ya Kaskazini, mkoani Arusha leo Heche amesema tayari chama hicho kimewashirikisha wadau mbalimbali kuhusu ajenda hiyo na kwamba wataipeleka mbali zaidi.
“Ajenda yetu no reform, no election inazungumzika hata kama wanaizungumzia negatively (kwa mtazamo hasi) lakini wanazungumza ajenda ya CHADEMA, tumetoka na ajenda hiyo ndiyo kila siku Wasira anaimba na leo ndio Makala alikuwa anaizungumza” amesema Heche.
“Sisi ni watu tunatumia brain (akili) tume engage (kushirikisha) tumeandika mapungufu 16 ya uchaguzi ambayo hayamuwezeshi mpinzani yoyote kushinda uchaguzi, nani miongoni mwenu anaweza kusema kwamba anaweza kushinda uchaguzi kwa utaratibu huu tulionao?” amehoji Heche
“Tumewaona viongozi wa dini tumezungumza nao na tumewapelekea ripoti ya mapungufu na nini tunachotaka ili twende kwenye uchaguzi, tumeonana na NGO na tutaonana na mashirika ya kimataifa ndani nan je ya nchi na Mwenyekiti wetu hivi karibuni atakuwa nje ya nchi ku engage” amesema Heche.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED