Tunairudisha DAWASA kwa wananchi- Mhandisi Bwire

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:51 PM Feb 20 2025

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire.
Picha: Mpigapicha Wetu
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire amesema wanakusudia kurejesha Mamlaka hiyo kwa wananchi ili kutoa fursa na na nafasi ya kufikisha mrejesho wa huduma na kutatua changamoto za Maji ili kusaidiwa kwa haraka.

Mhandisi Bwire ameyasema hayo leo Februari 20, 2025 wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi kati ya DAWASA na Wenyeviti wa mitaa wa Wilaya ya Temeke na kusema kuwa hiyo ndio agenda ya mamlaka katika utendaji kazi wao

“Tunekusudia turudishe DAWASA iwe ni ya wananchi tunaamini tukishirikiana pamoja changamoto za  kihuduna kupitia Wenyeviti wa mitaa zitaisha” amesisitiza Mhandisi Bwire

Mhandisi Bwire amesema kupitia kikao hicho watajadili changamoto za maji zilizopo katika maeneo ya Temeke kupokea mawazo na maoni ya wenyeviti juu ya suluhisho lakini kujenga mahusiano yatakayosaidia kuweza kuwa karibu baina ya DAWASA na viongozi hao.

“Lazima tuwe na mambo ambayo tunataka kushirikiana na kujenga uelewa wa pamoja tunapoenda kwa Wananchi kile anachozungumza Mwenyekiti na DAWASA azungumze hivyo” amesisitiza

Aidha Mhandisi Bwire ameongeza kuwa mamlaka hiyo imetambua umuhimu wa wenyeviti na kuelewa nafasi yao katika kurahisisha ufikishaji wa huduma kwa Wananchi na kutatua changamoto zilizopo

Pamoja na hayo Mhandisi Bwire amekiri uwepo wa changamoto mbalimbali katika Manispaa ya Temeke lakini amesema anaamini sasa itakuwa rahisi kutatua changamoto hizo kutokana na uwepo wa uhusiano mzuri baina yao.