Waziri wa Maji, Juma Aweso na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mha. Mwajuma Waziri wamekutana na Balozi wa Hungary mwenye makazi yake Nairob Kenya Zsolt Meszaros akiwa na ujumbe kutoka Hungary.
Kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za DAWASA Dar es Salaam kimelenga kupanua wigo wa Mashirikiano na Serikali ya Hungary hususani katika sekta ya Maji.
Aidha, Balozi huyo ameeleza ya Kwamba nchi yake inatoa mikopo isiyokuwa na riba kupitia programu ya Hungarian Tied End Credit, l Balozi Zsolt akifafanua zaidi amesema kupitia programu hiyo Tanzania itanufaka eneo la uwekezaji kwenye sekta ya Maji.
Katika hatua nyingine, Waziri Aweso amemueleza Balozi ya kuwa Wizara ya Maji ipo tayari Kwa ajili ya Mashirikiano katika kuhakikisha lengo la kumtua Mama ndio kichwani linatimia kwani ndio kipaumbele cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED