RAIS Samia Suluhu Hassan ameagiza vyombo vya uchunguzi kumpelekea taarifa ya mauaji ya Kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mohamed Ali Kibao.
Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa Septemba 8,2024 katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii ametoa maelekezo hayo akieleza kusikitishwa kwa tukio hilo.
"Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA, bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki,"
"Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana haki ya kuishi. serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii,".
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED