Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amemuagiza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Daniel Sillo kuwaachia huru Viongozi wote wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wanaoshikiliwa na Polisi Jijini Mbeya.
Dk. Nchimbi ametoa agizo hilo katika Mkutano uliofanyika wilayani Geita wakati akizungumza na Wakazi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro, Geita ambapo amemuelekeza Naibu Waziri Sillo kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ili Viongozi hao wa CHADEMA waachiwe huru.
“Kwakuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani upo hapa, mambo ya sheria sio ya kutolea maelekezo Kiongozi wa Chama cha siasa lakini nitumie nafasi hii mwambie Waziri wako kwamba tunaomba muone uwezekano wale Viongozi wa Vyama vya siasa waachiliwe ili mtupe nafasi ya kuzungumza nao kwasababu tunajenga Taifa moja tunapenda kuwa na Taifa tulivu kama kuna maeneo wamekosea wao au tumekosea sisi tukae tuzungumze tuijenge Nchi yetu” Dk.Nchimbi.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED