KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla, ametoa pole kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kufuatia kifo cha mjumbe wa Sekretarieti, Ally Kibao aliyeuawa na watu wasiojulikana.
Kada huyo aliwawa baada ya kutekwa na watu wasiojulikana akiwa kwenye basi kuelekea mkoani Tanga,kisha mwili wake kukutwa umetupwa eneo la Ununio,Dar es Salaam.
"Sisi vyama vya siasa linapokuja suala la ubindamu siasa unaweka kando,niomba jeshi la polisi.litimiza wajibu wake wa uchunguzi wa jambo hili,"alisema Makalla.
Alisema anatoa pole hizo kwa niaba ya CCM na kwamba utu ni kipaumbele.
Makalla alitoa pole hizo wakati akihutubia wananchi wa wilaya ya Simanjiro katika eneo la Mererani,ikiwa ni sehemu ya ziara yake mikoa ya Arusha na Manyara.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED