Asilimia nane ya wanawake Kigoma wana viashiria vya saratani

By Adela Madyane , Nipashe
Published at 11:16 AM Apr 23 2024
Kulia ni mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma Jesca Leba akiwa na katibu tawala wa mkoa Hassan Tugwa (katika), kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kigoma Salum Kalli katika uzinduzi wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi katika sekondari ya Msimba.
PICHA: ADELA MADYANE
Kulia ni mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma Jesca Leba akiwa na katibu tawala wa mkoa Hassan Tugwa (katika), kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kigoma Salum Kalli katika uzinduzi wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi katika sekondari ya Msimba.

IMERIPOTIWA kuwa asilimia nane ya wanawake wa Mkoa wa Kigoma waliofanyiwa uchunguzi wa awali wa saratani ya mlango wa kizazi kwa mwaka 2023 wamegundulika kuwa na viashiria vya ugonjwa huo.

Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Jesca Leba katika uzinduzi wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana kati ya umri wa miaka tisa hadi 14 uliofanyika katika sekondari ya Msimba iliyopo halamsahauri ya wilaya ya Kigoma.

Mganga Mkuu ametaja sababu za kuenea kwa ugonjwa huo kuwa ni pamoja kufanya mapenzi katika umri mdogo, kunywa pombe kali, kuvuta sigara na kuwa na mahusiano na watu wengi.

“Natoa rai kwa wanawake kuchukua hatua mapema kupima ugonjwa wa saratani, ikukumbuke kuwa saratani haina tiba, tiba ni kupata chanjo mapema na kuacha kuendeleza tabia hatarishi zinazosababisha ugonjwa huo na kwa watakaobainika kuwa na viashiria wapewe matibabu ya awali” amesema Leba.

Akizungumzia chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi iliyozinduliwa kimkoa jana amesema jumla ya mabinti 231,248 watachanjwa katika vituo 322 na kwamba chanjo zilizowafikia kwaajili ya zoezi hilo ni chanjo 280000