Sonko ateuliwa kuwa Waziri Mkuu Senegal

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:39 AM Apr 03 2024
Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko.
Picha: Seyllou/AFP
Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko.

RAIS mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amemteuwa kiongozi maarufu wa upinzani Ousmane Sonko, kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, baada ya kuapishwa kuwa Rais rasmi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Oumar Samba Ba, ametangaza uteuzi huo wa Sonko kupitia agizo la Rais lililopeperushwa kwenye kituo cha televisheni cha umma RTS.

Akizungumza baada ya kuteuliwa kwake, Sonko amesema kuwa atawasilisha kwa Rais orodha kamili ya mapendekezo ya uteuzi wa mawaziri ili kuidhinisha.

Sonko ameongeza kuwa hatamuacha Rais kukabiliana na jukumu hilo zito peke yake.

Sonko alikuwa mpinzani wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Macky Sall, ni maarufu miongoni mwa vijana nchini humo alizuiliwa kugombea katika uchaguzi wa urais wa Machi 24 kutokana na mashtaka yaliyokuwa yakimkabili na kujiharibia sifa. Hata hivyo alikanusha madai hayo.

DW