WHI wapewa tuzo ya nyumba nafuu Afrika

By Beatrice Moses , Nipashe
Published at 11:00 PM Oct 23 2024
Watumishi Housing Investments (WHI) yashinda Tuzo ya Nyumba ya gharama nafuu zaidi Afrika.
Picha: Mpigapicha Wetu
Watumishi Housing Investments (WHI) yashinda Tuzo ya Nyumba ya gharama nafuu zaidi Afrika.

Watumishi Housing Investments (WHI) yashinda Tuzo ya Nyumba ya gharama nafuu zaidi Afrika.

Mkurugenzi wa WHI Dk. Fred Msemwa amesema tuzo hiyo wamepewa na  Taasisi ya Mikopo ya Nyumba Afrika (Africa Union for Housing Finance-AUHF) inayo tambuliwa na Umoja wa Afrika (Africa Union).

 Tuzo hiyo imetolewa katika Mkutano Mkuu wa AUHF mwaka 2024 uliofanyika Zanzibar hivi karibuni. 

"Tuzo hii ya heshima inatambua jukumu la WHI katika kuwezesha umiliki wa nyumba kwa watu wa kipato cha chini na kati nchini, juhudi zilizofanywa na WHI za mfumo wa malipo za nyumba, ikiwemo malipo endelevu yanayolipwa kipindi cha ujenzi bila riba pamoja na utaratibu wa mpangaji mnunuzi,"amesema Dk. Msemwa. 

Amesema WHI  imejenga na kuuza/kukopesha 1000 hadi sasa, bado  wanaendelea kujenga katika maeneo tofauti. 

Afisa Masoko Mwandamizi wa WHI Maryjane Makawia,amesema kuwa taasisi hiyo imetajwa kuwa na vigezo rafiki kwa wanunuzi/wakopaji wa nyumba ikiwamo masharti nafuu. 

"Njia hizi zimeleta unafuu mkubwa sana kwa watu wanaotamani kumiliki nyumba.  Nyumba za WHI zinauzwa kwa bei nafuu kwa kati ya asilimia 10 hadi 30% ikilinganishwa na nyumba kama hizo kwenye soko, huku bei ya kununua nyumba ikianzia shilingi  milioni 38," anasema.

 Makawia,amesema bei hizi pamoja na njia nafuu za malipo ni wazi zimewasaidia watumishi wengi kufikia ndoto zao za kumiliki nyumba.

Tuzo hii pia inasherehekea kipindi maalum kwa WHI, kwani inatimiza miaka 10 ya ubunifu na uongozi katika sekta ya Makazi.
WHI inakuwa taasisi ya kwanza nchini na Afrika Mashariki kupokea Tuzo hii ya heshima. 

WHI iliibuka kinara kutoka kwa taasisi mbalimbali zinazohusiana na sekta ya makazi kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika. Tuzo za AUHF zinatambua michango thabiti ya kuendeleza sekta ya makazi barani Afrika. Ushindi wa WHI ulitokana na utekelezaji wake wa kipekee katika kubuni na kutekeleza miradi ya nyumba yenye gharama nafuu zaidi na hivyo kuleta unafuu kwa wanunuzi ikiwalenga watumishi wa umma na wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.

Aidha, tathmini ilihusisha kuangalia kazi halisi iliyotekelezwa na WHI, pamoja na mazungumzo ya moja kwa moja na wanufaika wa miradi yake. 

AUHF, shirika muhimu linalounganisha wadau wa makazi barani Afrika kwa zaidi ya miaka 40, linawezesha washirika wake kuendeleza ufumbuzi zaidi wa makazi ya bei nafuu.