Vizuizi vya jotoardhi kupatiwa uvumbuzi

By Beatrice Moses , Nipashe
Published at 09:38 PM Oct 23 2024
NAIBU  Waziri wa Nishati Judith Kapinga
Picha:Mpigapicha Wetu
NAIBU Waziri wa Nishati Judith Kapinga

NAIBU Waziri wa Nishati Judith Kapinga amesema ufumbuzi vizuizi vinavyozuia maendeleo rasilimali ya jotoardhi nchini utapatikana.

Amesema mjadala unaoendelea kwenye Kongamano la 10 la Joto ardhi lilililozinduliwa rasmi leo Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango linaweza kutoa suluhisho kukabili vizuizi hivyo. 

Wizara ya Nishati Kwa Sasa imejikita katika kutekeleza miradi mitano ya kipaumbele ambayo ni Ngozi (MW 70) Kiejo-Mbaka(MW60)  mkoani Mbeya na Songwe (MW5)Luhoi (MW5) Pwani na Natron (MW60) Arusha.

Kwa upande wake Mbunge George Mwenisongole wa jimbo la Mbozi akiwawakilisha wabunge wanaotoka kwenye mikoa yenye rasilimali ya jotoardhi amesema wananchi wanaoishi kwenye maeneo yenye miradi husika wapewe kipaumbele cha kupewa umeme usipitishwe kwenda maeneo mengine kabla ya wao kupata huduma hiyo. 

 Mbunge wa Nicholas Ngasa wa jimbo la Igunga alisema juhudi za serikali zinatoa  tumaini  kwa kuwa  inaonyesha nia ya wazi ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kukomesha adha ya kukatika umeme. 

Katika Mkutano  huo wa 10 wa Jotoardhi ambao unafanyika kwa mara ya pili nchini utafanyika kwa siku tatu, Mwakilishi wa Mkurugenzi  wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango la Mazingira (UNEP)Dk. Mesert Zemedkun  amekabidhiwa tuzo ya ushiriki wa kuendeleza matumizi ya jotoardhi. 

Pia Dk.Zemedkun amekabidhi uratibu wa jukwaa la jotoardhi kwa  Rais wa Shirikisho la Jotoardhi Afrika (AGA)Peter Omenda.