Jeshi la Zimamoto Kinondoni lawanoa wafanyakazi The Guardian

By Mary Kadoke , Nipashe
Published at 09:00 PM Oct 23 2024
Ofisa Habari Uhusisiano kwa umma wa jeshi hilo,  Sajenti Aman Hassan.
Picha:Mary Kadoke
Ofisa Habari Uhusisiano kwa umma wa jeshi hilo, Sajenti Aman Hassan.

Jeshi la Zimamoto na Uokoji Mkoa wa Kinondoni leo Oktoba 23, 2024, limetoa mafunzo ya uokoaji kwa wafanyakazi wa Kampuni ya The Guardian LTD.

Mafunzo hayo yametolewa na Ofisa Habari Uhusisiano kwa umma wa jeshi hilo,  Sajenti Aman Hassan ili kutoa elimu ya kinga, na uokoaji kipindi wanapopata majanga ya moto.

Katika mafunzo hayo, wafanyakazi walijifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na majanga ya moto, ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi ya vifaa vya kuzima moto na mbinu za kujiokoa. 

“Mafunzo hayo yamelenga kuimarisha usalama kazini na kuongeza uelewa wa namna ya kuchukua hatua za haraka na sahihi pindi hatari ya moto inapotokea ili kupunguza madhara na kuokoa maisha na mali katika mazingira ya kazi,” amesema Sajenti.

Aidha, amewahimiza wafanyakazi kuendelea kufanya mazoezi mara kwa mara na kuhakikisha vifaa vya kuzima moto vipo katika hali nzuri na vinapatikana kwa urahisi.