MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Uchimabji Madini ya MPP Mhandishi Ulimbakisya Spendi, ametoa wito kwa serikali kuyasaidia makampuni ya wanzawa kushindana na ya nje, akieleza kuwa wenzao wanafedha nyingi na teknolojia kubwa.
Akizungumza leo mkoani Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji wa Madini 2024, Mhandisi Spendi amesema serikali inatakiwa kuchukua hatua za makusudi za kuhakikisha kwamba inazilea kampuni ndogo wa Tanzania zikue na kumudu vizuri uchumi wao.
Pia amesema madini yanachangia sana katika kukuza uchumi wa taifa na wao kama wazawa ni muhimu kushiriki katika uchangiaji wa pato la taifa.
“Kwa sasa kuna asilimia 9.3 ya uchumi ambayo inatokana na madini lakini malengo yetu ni kwamba hadi ikifika 2025 nchi iweze kufaidia kwa asilimia 10 ya GDP,” amesema.
Ameongeza kuwa hitaji lao kubwa ni kuwezeshwa zaidi licha ya serikali kuwapunguzia kodi jambo ambalo limewasaidia kuongeza kipato na kuwawezesha wananchi kupata fedha.
“Ukipunguza kodi za serikalini inamaana utakuja kuongeza mishahara ya wafanyakazi na familia moja kwa moja zitapata faida,” amesema.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED