Uchaguzi wa wajumbe Mwangaza waahirishwa kufuatia kifo cha mgombea CCM

By Augusta Njoji , Nipashe
Published at 08:09 PM Nov 21 2024
Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Jiji hilo,  Dk. Frederick Sagamiko.
Picha: Mtandao
Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Jiji hilo, Dk. Frederick Sagamiko.

UCHAGUZI wa nafasi ya Wajumbe kundi la Mchanganyiko katika Mtaa wa Mwangaza jijini Dodoma umeahirishwa kufuatia kifo cha mmoja wa mgombea wa nafasi hiyo Christian Chawene.

Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Jiji hilo,  Dk. Frederick Sagamiko, amesema Mgombea wa nafasi ya Ujumbe kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) alifariki Dunia Novemba 11, 2024 baada ya uteuzi wa wagombea kufanyika.

Amesema kutokana na hali hiyo  Mitaa 221 badala ya 222 kwa nafasi za wajumbe Mchanganyiko ndio itafanya uchaguzi.

"Kwa mujibu wa Kanuni Namba 21 ya Kanuni za Uchaguzi Mamlaka za Mitaa, ngazi ya Miji inamtaka Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kuahirisha uchaguzi wa nafasi hiyo katika Mtaa husika na Chama cha Siasa kilichotoa Mgombea aliyefariki kitaweza kuwasilisha jina la Mwombaji mwingine ndani ya Siku 40 tangu kuahirishwa kwa uchaguzi, ili hatua za uteuzi kwa mwombaji huyo zifanyike,"amesema.