Kituo watoto yatima Raya Islamic chapewa msaada

By Faustine Feliciane , Nipashe
Published at 05:13 PM Nov 21 2024
Mkurugenzi wa Tigo-Mashariki na Pwani (Tanga na Morogoro) akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha kulea watoto wanaoishi mazingira magumu Raya Islamic Foundation, Subaha Maulid Shabani kilichopo Mvomero mkoani Morogoro.
Picha: Mpigapicha Wetu

KITUO cha kulelea watoto yatima Raya Islamic cha Mvomero mkoani Morogoro leo kimepokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka Kampuni ya Tigo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo kwa mikoa ya Morogoro,Pwani na Tanga, Abdully Ally, amesema msaada huo ni sehemu ya dhamira ya kampuni hiyo kushirikiana na jamii inayowazunguka ili kuimarisha maisha ya wale walio na uhitaji mkubwa.

Msaada uliotolewa ni pamoja na Mifuko ya sukari (kg 25 kila mmoja) mifuko nane ya mchele (kg 25 kila mmoja), mifuko 20 ya sabuni ya unga,mifuko 10 ya unga wa mahindi (kg 25 kila mmoja), ndoo tano za mafuta ya kupikia (lita 20 kila moja), mifuko mitano ya unga wa ngano, mifuko minne ya maharage (kg 25 kila mmoja) na vinginevyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kituo hicho,  Raya Maganga aliishukuru kampuni hiyo kwa moyo wa ukarimu na akasisitiza kuwa kutoa kwa wenye uhitaji ni njia ya kujitengenezea akiba ya fadhila.

1