Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya amezindua rasmi zoezi la utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake , vijana na watu wenye ulemavu , ambazo ni fedha za mapato ya ndani ya halmashauri na kutoa mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 817,619,365.
Uzinduzi huo umefanyika Jumatatu tarehe 18 Novemba katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi ( Ifakara FDC) uliopo uliopo Halmashauri ya Mji Ifakara
" Nawapongeza sana Vikundi vyote , Fedha hizo mkazitumie kulingana na Malengo mliyojiwekea . Halmashauri inaenda kutoa Fedha Milioni 817, 619,365 kwa makundi matatu , Wanawake , Vijana na Watu wenye Ulemavu, mkazitumie vizuri Ili mkatimize Malengo yenu" . alisema Kyobya
Wakati huohuo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara, Witness Kimoleta aliwasihi wote walioomba na watakaopata Mikopo hiyo kuzingatia kanuni, taratibu na Sheria za Mikopo ili ikatoe matokeo chanya katika shughuli wanazoenda kuzifanya na kutimiza azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha makundi mbalimbali ya wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu yanajikwamua kiuchumi.
"Tumewaandaa Maafisa wanaoshughulikia Mikopo kuendelea kutoa Elimu na kuwatembelea mara kwa mara katika maeneo yao kuhakikisha shughuli wanazofanya zinaleta tija". alisisitizaKimoleta na kuongeza
" Kiasi cha Sh. Milioni 261,000,000 kitatolewa kwa Kata 15 kati ya 19 kwa Vikundi vilivyokaguliwa na kukidhi vigezo kwa awamu ya kwanza , awamu nyingine zinafuatia, Halmashauri ya Mji Ifakara iko bega kwa bega na Wananchi kuhakikisha kwamba wanatumia Mikopo vizuri na Mikopo hiyo inaleta Mabadiliko katika maisha yao". alimaliza Kimoleta
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED