ZAO la Tumbaku ambalo katika msimu wa 2022/2023 limeshika nafasi ya kwanza katika kuliingizia taifa mapato ya fedha za kigeni hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu limeingiza Dola za Marekani milioni 394.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania,Stanley Mnozya, amesema hayo leo (April 17, 2024) wakati wa mkutano wa mwaka 2024 ambao unawashirikisha washiriki kutoka mikoa inayozalisha tumbaku ambayo ni Iringa,Ruvuma,Katavi,Tabora,Kigoma,Shinyanga,Singida,Mara,Geita,Kagera,Morogoro na Mbeya.
Alisema zao la Tumbaku lina mchango mkubwa katika maendeleo ya nchini ambapo kutokana umuhimu huo mkubwa uliifanya serikali kutoa agizo la kuongezwa kwa uzalishaji wa zao hilo hadi kufikia kilo 200,000,000 ifikapo mwaka 2025.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida,Godwin Gondwe ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida,Halima Dendego, amesema serikali inatambua umuhimu wa zao la Tumbaku katika kukuza pato la taifa hivyo kwa kuzingatia kuwa zaidia ya asilimia 70 ya watanzania wanategemea kilimo na kilimo ni uti wa mgongo kuna umuhimu wa kuwekeza katika mazao ya biashara pamoja na mazao ya chakula ili kuimarisha uchumi wetu
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED