Benki ya Maendeleo (TIB) kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) chini ya usimamizi wa Meneja wa SIDO mkoa wa Dar es Salaam Hopeness Elia wameendesha warsha fupi kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo waliolelewa na kukuzwa na Shirika la SIDO juu ya fursa za mikopo nafuu ya wajasiriamali ipatikanayo katika Benki ya Maendeleo TIB.
Warsha hiyo imefanyika Jijini Dar es salaam iliyohudhuriwa na wafanyabiashara wapatao 40 kutoka zekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Viwanda, Kilimo, Ujenzi, Usafirishaji wa bidhaa nje nchi, na Afya.
Mwakilishi wa Meneja wa TIB Kanda ya Dar es Salaam Eugene Naftal Ingwe amesema Benki ya TIB iko tayari kusikiliza mawazo yao na kuwashauri kitaalamu kwani Benki hiyo inakitengo maalumu cha wataalamu wa majengo na ufundi wa miradi.
Ameendelea kwa kuwafafanulia wajasiriamali hao kuwa wakisha kamilisha vigezo vyote vinavyotakiwa watawatembelea katika miradi yao na mengine yataendelea kulingana na miradi yao ilivyo kwa kuwa Benki hiyo ya TIB ina fursa mbalimbali za mikopo ya SME ipatikanayo katika Benki hiyo.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED