Mahakama Kuu ya Tanzania Kituo cha Usuluhishi imetoa tuzo ya 'Stakeholders Recognition Awards' kwa taasisi, majaji, mahakimu na vituo binafsi zilizofanya vizuri kwenye kuendesha mashauri yao kwa njia ya usuluhishi.
Tuzo hizo hutolewa kwa vigezo mbalimbali ikiwemo kuwa na idadi kubwa ya kesi ambazo ziliamuliwa kwa njia ya usuluhishi, ubunifu, uweledi na njia zilizotumika wakati wa kuendesha mashauri.
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kupitia idara ya sheria umepokea tuzo hiyo kwa kuzingatia vigezo vyote vilivyowekwa na kwa kuthamini mchango wake katika kuendesha mashauri kwa njia ya usuluhishi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED