Doris Mollel Foundation yapendekeza wiki 40 za uangalizi kwa watoto njiti

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:46 PM Jan 17 2025
Doris Mollel Foundation 
yapendekeza wiki 40 za
 uangalizi kwa watoto njiti.
Picha:Mpigapicha Wetu
Doris Mollel Foundation yapendekeza wiki 40 za uangalizi kwa watoto njiti.

Taasisi ya Doris Mollel imetoa mapendekezo kwenye muswada wa marekebisho ya sheria za kazi (No. 13 2024), ambapo imependekeza iwapo mama atajifungua mtoto kabla ya muda wa kujifungua haujatimia (mtoto njiti), basi mama apewe muda wa wiki 40 za uangalizi wa mtoto badala ya wiki 36 zilizopendekewa katika muswada.

Kwa kuzingatia hilo, pia taasisi hiyo imependekeza mama apewe likizo ya uzazi, ambayo haitaathiriwa na muda wa uangalizi mtoto, ambao ni kabla ya kukamilisha wiki 40.

Katika taarifa yake baada ya kuwasilisha muswada huo bungeni Januari 14, 2025, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete amesema serikali inapambana kutatua changamoto zinazowakabiri kina mama wanaojifungua watoto njiti, ikiwemo kuweka miongozo rafiki.

1


Taasisi ya Doris Mollel ni shirika kinara wa Mtandao wa Afya ya Uzazi, pamoja na Mtandao wa Wazazi Wenye Watoto Njiti nchini, ambapo imekuwa ikiiomba serikali ifanye marekebisho kwenye sheria ya likizo ya uzazi tangu mwaka 2017.
2