DC Okash ateta na wazee Chemba

By Julieth Mkireri , Nipashe
Published at 08:20 AM Sep 22 2024
MKUU WA Wilaya ya Chemba Halima Okash
Picha: Mpigapicha Wetu
MKUU WA Wilaya ya Chemba Halima Okash

MKUU WA Wilaya ya Chemba Halima Okash amekutana na baadhi ya Viongozi wa dini na Wazee maarufu Wilaya ya Chemba ambao wameahidi kufanya uhamasishaji wa wananchi kujiandikisha pamoja na kupiga kura kupata viongozi bora.

Kikao hicho ni cha kwanza kwa makundi hayo tangu Okash ahamishiwe kuendelea na majukumu yake ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba akitokea Wilaya ya Bagamoyo.

Katika kikao  hicho Okash  aliwaomba wazee hao na Viongozi wa dini kutumia nafasi zao kuhamasisha wananchi kujiandikisha daftari la kudumu la mpga kura sambamba na kujitokeza kupiga kura kuchagua viongozi wao.

Pia aliwakumbusha kuisemea Serikali katika maeneo yao kuhusiana na mambo mazuri yaliofanywa ikiwemo miradi ya maendeleo ambayo imeleta mabadiliko ukilinganisha na Hali ilivyokuwa awali.

Kadhalika Okash amewataka wazee hao kuendelea kusimamia Mila na tamaduni za mtanzania kwenye maeneo yao ili kuepusha tatizo la mmong'onyoko wa maadili katika jamii,

1

Mmoja wa viongozi wa dini walioshiriki kikao hicho  Omari Said amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuwakutabisha na kujadili mambo mbalimbali huku akiahidi kushirikiana na Viongozi kuhamasisha wananchi kujiandikisha na kujitokeza kupiga kura.

Naye Halima Makeka amesema Mkuu huyo wa Wilaya amewapa heshima ya kuwasikiliza kupokea ushauri wao katika utendaji wake na kwa pamoja watadumisha ushirikiano huo kuhakikisha hakuna mipango inakwama