Trump aonya BRICS iwapo zitaachana na dola ya Marekani

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 03:17 PM Feb 02 2025
Rais wa Marekani, Donald Trump
Picha: Mtandao
Rais wa Marekani, Donald Trump

RAIS wa Marekani, Donald Trump, akiwa takribani wiki mbili katika IKULU ya White House, ameionya Jumuiya ya nchi zinazoinukia kiuchumi ya BRICS, kwamba zikiachana na matumizi ya dola yake, ataziwekea ushuru wa asilimia 100.

Amesema matumizi ya dola yake hayaepukiki na iwapo nchi hizo zitajiondoa katika matumizi ya dola kama njia ya malipo yake kimataifa, atiziongezea ushuru.

Nchi za BRICS zinajumuisha ambazo zinatoka Brazil, Russia, India, China na South Africana nyinginezo tano zilizojiunga hivi punde.

Amesema Marekani haiwezi tu kukaa kimya na kuangalia namna Jumuiya hiyo inavyofikiria kuachana na matumizi ya dola kama sehemu ya malipo yake kimataifa. 

Trump amesema inabidi Marekani ipate hakikisho kutoka kwa nchi za Jumuiya hiyo aliyosema zinaipinga Marekani, kwamba hazitounda sarafu mpya ya BRICS wala kutumia safaru nyengine yoyote kuchukua nafasi ya dola ya Marekani.

Rais huyo wa Marekani ameongeza kuwa iwapo nchi hizo zitachukua hatua hiyo basi zitatozwa ushuru kwa asilimia 100 katika bidhaa zao, na pia hazitoweza kuuuza na kununua bidhaa kutoka Marekani. 

Jumuiya hiyo ya BRICS inazijumuiya nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini. Mapema mwaka 2024 Iran, Misri, Ethiopia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) pia zilijiunga katika jumuiya hiyo, huku Indonesia ikijiunga nao mwanzoni mwa mwezi Januari.

Brics iliundwa ili kukabiliana na sarafu ya dola, na kama mbadala wa kundi la mataifa saba yaliyoendelea kiuchumi duniani ya G7. 

Rais wa Russia, Vladimir Putin amekuwa mara kwa mara akikosoa utegemezi wa dola ya Marekani na kutangaza nia yake ya kuanzisha mfumo huru wa malipo ndani ya Jumuiya ya BRICS.

DW