BODI ya Chai Tanzania (TBT), imesema lengo kuu ni kupanga kufikia malengo waliyojiwekea kuendeleza zao hilo, kwa muda wa miaka 10 kuanzia mwaka 2024 mpaka 2034.
Kaimu Mkurugenzi Bodi hiyo, Beatrice Banzi, amesema hayo alipokutana na wadau wa zao hilo nchini, kujadili pamoja namna ya kukabiliana na changamoto zinazokwamisha ustawi wa zao hilo.
Amesema mbali na hilo zipo baadhi ya changamoto zinazokwamisha zao hilo, pamoja na kukatika kwa umeme, ubovu wa miundombinu, ikiwamo barabara.
Bodi hiyo ilikutana na wadau kutoka serikalini, na bodi hiyo, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bandari, watu wa ushirika na Wizara ya Kilimo,.
Ameeleza kwamba TBT katika uimarishaji wa zao hilo, imeweka mikakati ya masoko ya chai akisema linahitaji uzalishaji wa kutosha na masoko ya kimkakati yaliyopo.
“Pia tutajadili namna ya kuongeza ubora wa chai, ili kulishika soko la chai ndani na je ya nchi, tutafanya hamasa kwa Watanzania kunywa chai kwa wingi na hasa inayozalishwa hapa nchini.”
“Lengo kuu ni kupanga kufikia malengo waliyojiwekea kuendeleza zao hilo, kwa muda wa miaka 10 kuanzia mwaka 2024 mpaka 2034.
Lakini ili kufikia malengo hayo, lazima watu wa serikali, sekta binafsi waweze kukaa chini kwa pamoja kujadili ni jinsi gani wanaweza kuokoa zao hilo.
“Hapa ni kama tunafanya ‘road map’, ili tuweze kujua tunaendaje, kama ni kuongeza uzalishaji, wale wadau wanaohusika na uzalishaji tunapanga kwa pamoja tunafanyaje.
“Kama tuna taka kutangaza chai yetu ndani na nje ya nchi tunafanyaje kwashirikiana na TANTRADE kwa hiyo yale majadiliano yetu sisi washiriki wa mkutano ndiyo yatatumika, kuboresha huu mkakati ambao tumeupanga kuinua na kuendeleza zao la chai kwa hiyo miaka kumi,” amesema Beatrice
Aidha amesema katika kikao hicho, watatambulisha nembo ya chai ya Tanzania, ili iwe rahisi kutambuliwa hata ikiuzwa nje ya nchi na kwamba wanaamini hatua hiyo itasaidia kukuza biashara ya zao hilo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED