DRC yaamuru shughuli za Rwanda kidiplomasia kukoma

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 03:04 PM Jan 26 2025
Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Picha: Mtandao
Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

JAMHURI ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), imeamuru Rwanda kukomesha shughuli zake zote za kidiplomasia na za kibalozi nchini humo.

Imetoa muda wa saa 48. Hatua hiyo inaweza kuonekana kama kuongezeka kwa mvutano kati ya nchi hizo mbili.

Hatua hiyo inawadia wakati kikundi cha waasi cha Tutsi kinachoongozwa na M23, kuendelea na mashambulizi huko Goma, mji mkuu wa Kivu Kaskazini, DRC.

Mamlaka ya Congo na wataalam wa UN, wanaishtumu Rwanda kwa kuwasaidia waasi, ingawa Kigali imekanusha mashtaka hayo mara kwa mara.

"Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, imejitolea kuheshimu taratibu zote za kidiplomasia na kuhakikisha mabadiliko ya utaratibu ya uamuzi," Wizara ya Mambo ya Nje ya DRC ilisema katika taarifa.