Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amewasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria za Kazi (Na. 13) wa Mwaka 2024 (The Labour Laws Amendments (No.13) Bill, 2024) mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, jijini Dodoma, leo Januari 14, 2025.
Aidha, Waziri Kikwete amesema Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kusimamia uwepo wa mazingira mazuri ya kazi na kuhakikisha kwamba viwango vya kazi vinazingatiwa ili wananchi wafanye kazi zenye staha.
"Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliponiteua alielekeza moja ya jambo la kulisimamia ni pamoja na kuhakikisha wafanyakazi wanafanya kazi zenye staha, hivyo tutaifanya kazi hiyo," amesema Kikwete.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED