SHULE ya Msingi Buyuni iliyopo kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze imepata msaada wa madawati 70 kutoka Taasisi ya Alryyan Islamic Society of Tanzania.
Madawati hayo yametolewa baada ya Taasisi hiyo kupokea maombi ya Diwani wa Vigwaza Mussa Gama kuhusiana na mahitaji katika shule hiyo.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Gama ameishukuru Taasisi hiyo kwa kusaidia kupunguza kero ya upungufu wa madawati ambayo ilikuwa inawalizimu wanafunzi kukaa watano katika dawati moja.
Gama pia amesema pamoja na kupokea madawati hayo pia ameiomba Taasisi hiyo kusaidia upatikanaji wa viti vya walimu ombi ambalo waliahidi kulifanyia kazi.
Katika hatua nyingine Gama ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu sambamba na ujenzi wa shule ambazo zinawapunguzia watoto adha ya kutembea umbali mrefu.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED