Polisi atunukiwa kwa ushirikiano, karibu na jamii

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:01 PM Feb 05 2025
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Pius Lutumo (kushoto)
Picha: Mpigapicha Wetu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Pius Lutumo (kushoto)

POLISI Kata ya Ikoma Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Koplo Emmanuel Kisiri, ametunukiwa cheo cha Sajenti, kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi hasa ushirikiano na kujiweka karibu zaidi na jamii anayoihudumia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Pius Lutumo, alimvisha cheo hicho jana, Februari 4 mwaka huu katika viwanja vya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wilayani hapa.

Aidha, mara baada ya kumpandisha cheo hicho, Kamanda Lutumo alisema askari huyo anapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa ushirikiano na kujiweka karibu zaidi na jamii anayoihudumia.

oplo Emmanuel Kisiri apandishwa cheo kuwa sajenti
"Kutokana na jitihada alizozionyesha Koplo Emmanuel Kisiri ni dhahiri kuwa ana uwezo wa kuongoza hivyo anastahili kutunukiwa cheo cha Sajenti" amesema Kamanda Lutumo.

Akizungumza kwa furaha kubwa mara baada ya kupewa wadhfa huo Sajenti Kisiri, alisema anamshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Uongozi wa Jeshi la Mkoa wa Mara, wananchi wa Kata ya Ikoma na wadau mbalimbali, waliomfanikisha kutunukiwa cheo hicho.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Pius Lutumo amtunuku polisi
Kamanda Lutumo amemvisha cheo polisi kata ya Ikoma kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Camilius Wambura.