Precision Air, Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania wasaini mkataba wa mafunzo

By Imani Nathaniel , Nipashe
Published at 05:01 PM Feb 05 2025
Precision Air,  Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania wasaini mkataba wa mafunzo.
Picha: Iman Nathaniel
Precision Air, Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania wasaini mkataba wa mafunzo.

Shirika la ndege la Precision Air na Chuo cha Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania, wamesaini mkataba wa mashirikiano wa mafunzo wenye lengo la kutoa Elimu na ujuzi katika ngazi mbalimbali kwa Shririka la Precision Air Tanzania.

 Hafla hiyo ya utiaji saini imefanyika mapema leo 5 Februari 2025, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Precision Air jijini Dar es Salaam 

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Precision Air, Patrick Mwanri, amesema kuwa makubaliano hayo yanalenga kuboresha ufanisi wa huduma katika shirika hilo kuanzia ngazi ya Uongozi wa Wakurugenzi pamoja na wafanyakazi wa ngazi zote.  
"Mkataba huu tuliousaini leo utasaidia kuboresha mahusiano mbali na chuo cha Wakurugenzi Tanzania bali hata kimataifa itasaidia kuboresha ufanisi wa kazi na ubora wa huduma zetu kwa ujumla " amesema Mwanri.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa chuo cha Wakurugenzi Tanzania, Said Kambi, amesema kuwa ushirikiano huo unalenga kuinua maono mbalimbali juu ya Shirika hilo linaloendesha huduma za usafiri wa anga ndani na nje ya mipaka ya Tanzania .

"Chuo chetu kinalenga kuimarisha huduma mablimbali ambazo zinatanua mipaka ya Uongozi kuanzia ngazi za Ukurungenzi na Uongozi kwa ujumla." amesema Kambi.