Mwandishi wa Ayo TV hajulikani alipo, anatafutwa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:21 PM Jan 06 2025
 Eugene Peter.
Picha: Mtandao
Eugene Peter.

AYO TV kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii imetoa taarifa ya kupotea kwa Mwandishi wake Eugene Peter ambaye inadaiwa ametoweka bila kujilikana alipo akitimiza siku ya tisa leo pasipo kupatikana.

Familia pamoja na Ofisi yake ya AYO TV zinamtafuta Mwandishi huyo ambaye mara ya mwisho alionekana mazingira ya nyumbani kwake Jumapili December 29,2024 majira ya saa mbili usiku. 

Familia akiwemo Baba yake Mzazi na Watu wa karibu wamethibitisha kutokuwa na mawasiliano naye tangu wakati huo ambapo Dar es Saalam hajaonekana na kwao Arusha na Moshi hajafika huku simu zake zikiwa hazipatikani.

Baada ya jitihada kubwa za kumtafuta maeneo mbalimbali na kutoa taarifa ya kupotea kwake Polisi, AyoTV na Familia kwa pamoja wanaomba mtu mwenye taarifa kumuhusu apige simu namba 0748400047 au aripoti kituo cha Polisi kilicho karibu nae.

Kusoma habari hii zaidi tembelea epaper.ippmedia.com

#NipasheMwangaWaJamii #NipasheDigital