MBUNGE wa Arusha Mjini Mrisho Gambo ametoa ufafanuzi wa sakata lililoibuka jana baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda kumrushia maneno kwamba ametoa malalamiko ya kutaka kujengwa barabara ambayo imekuwa changamoto kwa wananchi huku Makonda akimkosoa kwamba suala hilo lilisha jadiliwa kwenye vikao vya ndani.
Sakata hilo liliibuka jana mkoani Arusha wakati Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega alipokuwa akikagua barabara ya Mianzini Ngaramtoni, ambako Gambo aliwasilisha hoja nne zilizohusu changamoto ya miundombinu ya barabara ambayo ilihitaji ufafanuzi ili wananchi waelewe.
Akifafanua kuhusu hoja hizo leo Gambo amesema, hoja ya kwanza Juni 16, 2023 walialikwa kwenda kushuhudia kusaini mkataba kupitia mradi wa IPC ambao ungejenga barabara ya Arusha Kibaya Kongwa wa Kilomita 453.4, ambayo jiji hilo na wenzo wa Arumeru wangenufaika kwa ujenzi kuanzia kona ya Mbauda hadi Bondeni City.
“Ujenzi huo ungesaidia kuondoa msongamano na mafuruko kwasababu wananchi wa Kata ya Sombetini na maeneo mengine wamekuwa wanateseka kwa muda mrefu, sasa tulisaini mkataba tangu 2023 lakini mpaka leo mkandarasi hayuko saiti.
“Waziri wa Ujenzi ndio mwenye dhamana kwahiyo nilitumia fursa hiyo kumuomba atoe ufafanuzi kwa wananchi wajue serikali imejipangaje kutekeleza mradi huo ambao mkatamba wake ulisainiwa hadharani na ukiangalia leo ni mwaka 2025 ni kipindi kirefu, tunahitaji kupata majibu kama wananchi,” amesema Gambo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED