MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amesema Siku ya Wanamke Duniani, mkoani humo itafana mwaka huu, ikiwa yenye tija kwa wanawake wa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla.
Makonda amesema kabla ya kilele Machi 8, mwaka huu, na kumpokea Rais Samia Suluhu Hassan, anayetarajiwa kuwa mgeni rasmi mkoani humo, kutakuwa na matukio mbalimbali kuanzia, Machi Mosi mwaka huu.
Mkuu wa mkoa huo, amesema hay leo katika kikao kazi cha maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Wanamke Duniani, kikihudhuriwa na wajumbe kutoka wizara mbalimbali, walishiriki kwa lengo la kuweka mikakati thabiti ya kuhakikisha maadhimisho hayo yanafanyika kwa ufanisi.
"Huduma hii itatolewa na madaktari bingwa wabobezi wa nyanja hii, lengo wanawake washerehekee siku yao kwa furaha na amani," amesema Makonda.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED