Kamati yaridhishwa na ujenzi wa maktaba Chuo cha Ardhi Tabora

By Augusta Njoji , Nipashe
Published at 09:34 AM Feb 11 2025
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeridhidhwa na ujenzi wa mradi wa maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) ambao umefikia asilimia 99 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Februari 2025.
Picha: Mpigapicha Wetu

Akizungumza wakati wa majumuisho mara baada ya ziara ya kukagua ujenzi wa maktaba hiyo mjini Tabora, Mwanyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Timotheo Mzava alisema kamati yake imejionea na kuridhishwa kwa hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa maktaba hiyo pamoja na maendeleo ya chuo hicho.

“Kwa ujumla Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii baada kupitia, kukagua, kupata taarifa na kujionea kwa macho, imeridhishwa na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na uongozi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja Chuo cha Ardhi Tabora katika kukamilisha jengo hili la maktaba” alisema 

Naye, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda aliishukuru kamati hiyo ambayo ndiyo yenye dhana ya kuisimamia, kushauri, kutoa maelekezo mbalimbali na kufuatilia kazi zinazotekelezwa na wizara hiyo.