WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Seleman Jafo amesema ndani ya siku 60 Wizara yake itakuwa imepata ufumbuzi wa malalamiko ya wawekezaju kuhusu tozo ya shilingi 150,000 wanayotozwa kwaajili ya kushusha na kupakia kontena.
Alitoa ahadi hiyo jana mara baada ya mkutano baina yake na wanachama wa Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), ambao wamekuwa wakilalamikia kutozwa shilingi 150,000 kwa kontena linaloshushwa na kupakiwa kwenye halmashauri hizo kutoka bandarini.
Alisema ni kweli wizara yake imepata malalamiko hayo ya tozo za kontena na wawekezaji wengi nd ndiyo sababu waliamua kukutana nao kuwasikiliza.
“Kwenye hili suala kuna sekta mbalimbali zinahusika kwa hiyo serikali itaratibu tukae pamoja tuangelie nini kifanyike tuwasaidie wafanyabiashara hawa na tumekubaliana kwamba ndani ya siku 60 tutakuwa tumepata jawabu la malalamiko haya,” alisema Waziri Jafo
Alisema malengo ya Rais Samia ni kuona viwanda vinafanya vizuri mwaka hadi mwaka na uwekezaji unaendelea kukua hivyo changamoto kama hizo kuna umuhimu wa kuzifanyia kazi kwa haraka.
“Na kwenye viwanda ndipo vijana wetu wengi wanaajiriwa kwasababu serikali zote duniani mwajiri mkuu ni sekta binafsi kwa hiyo serikali itatengeneza mazingira mazuri vijana wajiajiri au waajiriwe,” aliongeza Dk Jafo
Alisema ni mkakati wa serikali kuendelea kuweka mazingira mazuri kuhakikisha viwanda vinaendelea kukua na kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wanaohitimu kwenye fani mbalimbali vyuo vikuu.
“Suala hili ni mtambuka na ndiyo maana kwenye mkutano huu tulipanga kuwa na Waziri wa Fedha, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ili tuwasikilize kwa kuja na jawabu la pamoja lakini wamepata dharura ,” alisema
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI), Leodegar Tenga alisema shirikisho limefarijika kuona serikali imeamua kukaaa kuwasiliza wafanyabiashara dhidi ya malalamiko hayo.
Alisema tatizo hilo linaongeza gharama za uzalishaji kwa wafanyabiashara na wenye viwanda hali ambayo inawafanya washindwe kushindana kwenye soko.
“Tunataka maendeleo ya viwanda na maendeleo hayo yatakuwepo pale viwanda vitakapopata faida na kunapokuwa na ushindani wa haki kwa hiyo tunamshukuru waziri kwa kuamua kuja kwenye mkutano huu,” alisema na kuongeza
“Na kama Waziri alivyoahidi nasisi tunaaamini kwamba ndani ya siku 60 tutapata majibu ya tozo hizi. Tunajua faaida za viwanda vinalutea mapato ya serikali na ajira kwa hiyo utulivu na mafanikio ya viwanda ni mafanikio ya uchuimi wa nchi yetu,” alisema Tenga
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Toba Nguvila siyo kwamba tozo hizo zinatozwa kiholela bali ni halali kwasababu zimetokana na sheria ndogo ndogo za Manispaa za Temeke, Kinondoni, Ilala, Ubungo na Kigamboni.
Alisema Mkoa umeshaka vikao viwili na Shirikisho la Wenye Viwandakujadili namna ya kumaliza changamoto hiyo na kwamba baadhi ya changamoto zimeshapatiwa ufumbuzi na zingine zinaendelea kufanyiwa kazi.
“Changamoto ya tozo bado inafanyiwa kazi ili tupate mwisho mwema, Mkoa uko tayari na utaendelea kuwa tayari kukaa na wafanyabiashara hawa na kutatua changamoto hizi zinazowakabili,” alisema
“Hata Rais Samia Suluhu Hassan hapendi kusikia malalamiko ya wenye viwanda kwasababu sera yake ni kuinua maendeleo ya viwanda kwa hiyo sisi hatupaswi kuwa kikwazo kwa viwanda na badala yake tunatakiwa kuwa wawezeshaji,” alisema
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED