ACT , CHADEMA, CHAUMMA na CUF vyaungana kuikabili CCM

By Restuta James , Nipashe
Published at 03:48 PM Feb 11 2025
Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu.

CHAMA cha ACT Wazalendo kimesema kuwa kimeshafanya mawasiliano na vyama vyote makini kwa ajili ya kuungana kukikabili Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katibu Mkuu wa chama hicho,  Ado Shaibu,  aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa kwenye Jimbo la Kibiti akiwa anaendelea na ziara yake ya siku tatu katika majimbo matatu ya Mkoa wa Kichama wa Mwambao. 

Ado alisema tayari chama hicho kimeshazangumza na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi.
Alivitaja vyama hivyo na kueleza ndivyo vilivyokataa dhuluma ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika 2024.

Ado alisema huu ndio muda wa kuunganisha nguvu kuikabili CCM.