Kipindupindu chaiweka hatarini Goma

By Vitus Audax , Nipashe
Published at 01:09 PM Feb 12 2025
Kipindupindu waiweka hatarini Goma.
Picha: Mtandao
Kipindupindu waiweka hatarini Goma.

Wakati ghasia katika Mji wa Goma zikionekana kutulia na shughuli za kijamii na kibinadamu zikiendelea chini ya serikali mpya ya wanamgambo wa M23, ukosekanaji wa huduma ya Maji unauweka matatani Mji huo dhidi ya ugonjwa wa mlipuko wa kipindupindu.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa tangu kukatwa kwa huduma ya umeme na maji wakati wa vita bado wakazi zaidi ya milioni moja wa Mji huo wanapata shida hasa upande wa huduma ya maji.

Tayari M23 imeanzisha utawala wake huko Goma kwa kuteua magavana pamoja na Meya na wasaidizi wao, ikizindua kampeni za kuajiri, pamoja na kuunda jeshi la polisi.

Licha ya juhudi na mikakati hiyo ya M23 bado wakazi wake wapo matatani dhidi ya magonjwa ya mlipuko ambako wakaazi wanalazimika kuchukua maji kutoka Ziwa Kivu, ambapo miili iliopolewa mara baada ya mapigano.

Mgogoro katika Mashariki mwa DRC unatarajiwa pia kujadiliwa katika mkutano wa umoja wa Afrika huko Addis Ababa siku ya Ijumaa licha ya juhudi za EAC na SADC kutoleta mafanikio ya haraka ya usitishwaji wake.

Pamoja na kuongezeka kwa mzozo hivi karibuni, wito wa kuongezeka kutoka kwa jamii ya kimataifa umeongeza wakati wa hofu mapigano yanaweza kusababisha vita vya mkoa.

Lakini juhudi za kidiplomasia za kutatua mzozo ambao umedumu kwa zaidi ya miaka mitatu hadi sasa haukufanikiwa.

DRC imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuiwekea vikwazo Rwanda licha ya ombi hilo kutokuzingatiwa na upande wotete huku kila Taifa likionekana kutaka Suluhu ipatikane kwa maongezi.

Kinshasa anamshutumu Kigali kwa kutaka kupora rasilimali za asili katika DRC, kama vile tantalum na bati inayotumiwa katika betri na vifaa vya elektroniki, na dhahabu.

Rwanda imekanusha mara kadhaa suala hilo, ikisema inajilinda ikilenga kuondoa vikundi vyenye silaha ikiaamini kuwa tishio la kudumu kwa usalama wake, haswa vikosi vya Kidemokrasia kwa ukombozi wa Rwanda (FDLR), iliyoundwa na viongozi wa zamani wa Wahutu wa mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Tutsi nchini Rwanda.

Mizozo tofauti na uasi zimeumiza nchi hii kwa zaidi ya miaka 30.