ZANZIBAR inakabiliwa na uhaba wa madaktari bingwa wa maradhi ya moyo na kwa sasa inawatalamu sita kati ya hao, daktari mmoja ni wa upasuaji moyo na mtalamu mwingine wa dharura kwa magonjwa hayo.
Idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya watu Zanzibar, kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ina watu milioni 1.8.
Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, amesema kwa mwaka 2024 wagonjwa wa moyo 624 visiwani humo, wametibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwetwe (JKCI).
Alisema taasisi hiyo ina mchango mkubwa kwa serikali kwa sababu wagonjwa wengi wanaosumbuliwa na moyo na kushindikana kutubiwa Zanzibar, taasisi hiyo huwachukua na kuwatibu.
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Amour Suleiman Mohammed, alisema watoto vichanga wanaofariki yawezekana sio wote hufariki, sababu hakuna watalamu wenye ujuzi wa kurejesha uhai wao na huwenda ikawa moyo tu umesimama.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED