Francis Butoto (64), mkazi wa Kijiji cha Kishanda, Kata ya Kibare, Tarafa ya Murongo, Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, ameuawa na mwili wake kufukiwa kwenye shimo la choo lililokuwa likitumiwa kijana wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, SACP Brasius Chatanda, amesema mauaji hayo yalitekelezwa Februari 22, 2025, chanzo kikiwa ni mgogoro wa mali za familia. Watuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na mke wa marehemu, Frola Bitakalamile (42), George Bitaka (52), Detric George (19) na Christopher Bitakalamile (30).
Aidha, Kamanda Chatanda amefichua kuwa baada ya tukio hilo, wananchi wa eneo hilo walijichukulia sheria mkononi kwa kuharibu mali za familia ya Bitakalamile. Polisi wanaendelea kumsaka yeyote aliyehusika na vurugu hizo, huku orodha ya wahusika ikiwa tayari imeandaliwa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED