BENKI Kuu ya Tanzania BoT, imesema haijafanya mazungumzo wala kutoa maelekezo yoyote kuhusu kupewa leseni au kuruhusu kampuni inayoitwa LBL tofauti na taarifa zinazosambaa mtandaoni.
Imesema hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa na maofisa wa kampuni hiyo, kwa kujihusisha na ulaghai ikiwamo kupokea amana, kutoa riba na kufanya uhaurishaji wa fedha bila leseni ya BoT.
Aidha taarifa hiyo imeonya watu binafsi kujiepusha na taasisi, kampuni au mtu binafsi anayetoa huduma za kifedha bila leseni au wasimamizi wengine wa huduma za fedha.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED