RAIS Samia Sulluh Hassan amezindua shule ya wasichana ya Mkoa wa Tanga leo Februari 25 katika Kijiji cha Mabalanga wilayani Kilindi, ambayo inafundisha mchepuo wa sayansi.
Wakati akizindua shule hiyo Dk. Samia aliwaomba wananchi wilayani humo kuipa jina aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, hayati Beatrice Shelukindo ambaye pia alikuwa mpambanaji wa masuala ya wanawake.
"Kwahiyo nikuombe Mkuu wa Mkoa ikikupendeza, mmuite jina hilo, na alikuwa mpambanaji hata alipokuwa kwenye kuwania nafasi ile ya ubunge" amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED