BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imesema kuwa fedha zenye saini ya Gavana, Emmanuel Tutuba na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, zimeshaingia kwenye mzunguko nchini.
Ufafanuzi huo ulitolewa jana, kwa waandishi wa habari waandamizi wanaoshiriki semina kuhusu majukumu mbalimbali ya BoT katika masuala ya fedha na uchumi nchini.
Januari 22, mwaka huu, Gavana wa BoT, Tutuba alisema noti mpya zenye Saini zao (Gavan ana Waziri) zitaanza kutumika Februari Mosi, mwaka huu ikiwa ni toleo la mwaka 2010 ambazo ni za Sh. 10,000, 5,000, 2,000 na 1,000.
“Kazi yetu ya uchapaji upya wa noti kwa marejeo ya toleo la mwaka 2010, limekamilika na tayari tu=mewajulisha wananchi kupitia taarifa niliyoitoa kwenye Gazeti la Serikali,” alisema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED