MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara, John Heche amesema chama hicho kinataka viongozi kuwaheshimu wananchi ambao ndio wapigakura wao.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika mji wa Lamadi, mkoani Simiyu ikiwa ni mara ya kwanza tangu achaguliwe katika nafasi hiyo Heche amesema baadhi ya viongozi hawaheshimu kura za wananchi na hivyo kushindwa kuwahudumia ipasavyo.
“Tunataka viongozi waheshimu kura za wananchi, tunataka rasilimali za nchi hii zitumike kuwanufaisha wananchi” amesema Heche
“Kuna vijana wanagundua machimbo, lakini kesho yake wanakuja watu kutoka mjini wana lesini tayari, vijana wanaambulia kupigwa na polisi” amesema.
Amesema kutoka na kuishi maisha ya ukwasi kwa baadhi ya viongozi kumewafanya kushindwa kutambua tabu wanazopitia wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED