Aua mke, naye ajimaliza

By Ida Mushi , Nipashe
Published at 05:02 PM Feb 12 2025
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama
Picha: Mtandao
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama

HASSAN Mtawanja (40), fundi ujenzi na mkazi wa Kiembeni, wilaya ya Morogoro, anadaiwa kumuua mkewe Naria Abdallah (34 ), kisha naye kujiua, kisa wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, amesema tukio hilo limetokea katika mtaa wa Kiembeni, Kata na Tarafa ya Mikese, Wilaya ya Morogoro, kwamba mwanamke huyo ameuawa kwa kuchomwa kwa kitu chenye kali eneo la kifuani na mumewe.

Anasema mtuhumiwa baada ya tukio hilo, alijichoma sindano ya kushonea viatu tumboni na kisha kujiua kwa kujinyonga kwa kamba ya katani, ndani ya nyumba yao na uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha tukio hilo ugomvi uliosababishwa na wivu wa mapenzi. 

Kamanda Mkama anasema miili yote imehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospital ya Rufani Morogoro na kusubiri taratibu zaidi za mazishi.