Watu 1,300 wapoteza maisha katika Ibada ya Hija

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:20 PM Jun 24 2024
Zaidi ya watu 1,300 wamefariki dunia wakati wa ibada ya Hija.
Picha: Maktaba
Zaidi ya watu 1,300 wamefariki dunia wakati wa ibada ya Hija.

ZAIDI ya watu 1,300 wamefariki dunia wakati wa ibada ya Hija mwaka huu nchini Saudi Arabia huku waumini wakikabiliwa na hali ya joto kali katika maeneo matakatifu ya Kiislamu katika ufalme huo wa jangwani.

Waziri wa Afya wa Saudia, Fahd bin Abdurrahman Al-Jalajel, amesema kuwa asilimia 83 ya vifo hivyo, ni mahujaji ambao hawakuidhinishwa waliotembea umbali mrefu katika hali ya joto inayoongezeka, kushiriki ibada ya Hija ndani na karibu na mji mtakatifu wa Mecca.

Akizungumza na televisheni inayomilikiwa na serikali, Waziri huyo amesema mahujaji 95 walitibiwa hospitalini, huku baadhi yao wakisafirishwa kwa ndege kwa matibabu zaidi katika mji mkuu wa Riyadh.

Amesema mchakato wa kuwatambua watu hao ulichelewa kwa sababu ya kutokuwepo kwa vitambulisho kwa mahujaji wengi waliofariki dunia.

VOA Swahili