RAIS mteule wa Marekani. Donald Trump, amesema Rais wa Russia, Vladimir Putin, anahitaji kuonana nae mapema iwezekanavyo.
"Rais Putin anasema anataka kukutana nami haraka iwezekanavyo.
"Kwa hivyo itabidi tusubiri, lakini lazima tukomeshe vita hivi. Vita hivi vinatisha, vinatisha."Trump alisema katika kongamano huko Arizona. Trump, ambaye atarejea Ikulu ya White House, Januari, 2025, awali wakati wa kampeni alisema kwamba akichaguliwa kuwa rais anaweza kumaliza vita hivyo chini ya saa 24.
Hivi karibuni alikosoa uidhinishaji wa Biden kwa Ukraine kutumia silaha za masafa marefu zilizotolewa na Marekani kushambulia eneo la Russia.
BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED