MKUU wa Jeshi la Nigeria, Jenerali Taoreed Lagbaja (56), amefariki dunia baada ya kuugua.
Rais wa nchi hiyo Bola Tinubu, ametangaza juu ya kifo hicho.
Anaelezwa kuwa aliaga dunia usiku wa kuamkia leo, Novemba 06,2024 jijini Lagos.
Maelezo kamili kuhusu ugonjwa wake hayakutolewa.
CHANZO: BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED