Kenya yatuma Askari kutuliza ghasia Haiti

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:52 PM Jun 24 2024
Maafisa wa Polisi wa Kenya wakijaribu kuzima maandamano nchini Kenya.
Picha: Brian Inganga/AP Photo/picture alliance
Maafisa wa Polisi wa Kenya wakijaribu kuzima maandamano nchini Kenya.

KIKOSI cha Askari Polisi nchini Kenya, Kesho Jumanne Juni 25, 2024 kinatarajia kuondoka kuelekea Haiti ili kuongoza ujumbe unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kukabiliana na ghasia za magenge katika nchi hiyo ya Caribbean.

Kenya ilijitolea kutuma takriban polisi 1,000 watakaoungana na vikosi kutoka nchi nyingine ili kusaidia kuleta utulivu nchini Haiti, lakini hatua hiyo ilikabiliwa na changamoto za kisheria katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Rais William Ruto amekuwa akiunga mkono hatua hiyo ambayo inatiliwa mashaka na shirika la kimataifa la kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch hasa kuhusu ufadhili wake.

Mbali na Kenya, nchi nyingine ambazo zimeonyesha nia ya kujiunga na ujumbe huo wa kulinda amani Haiti ni pamoja na Benin, Bahamas, Bangladesh, Barbados na Chad.

DW