BAADHI ya mataifa yanayoendelea yamekosoa ofa ya ufadhili wa hali ya hewa ya uliofikia dola bilioni 300, yakisema ofa hiyo inashindwa kufikia kiwango, kulingana na changamoto watazokabiliana nazo katika miaka ijayo.
Muda mfupi baada ya makubaliano hayo kupitishwa mapema huko Baku, Azerbaijan, kundi la Afrika la Wapatanishi, Kambi ya Mataifa Yanayoendelea yenye Ushawishi, yalielezea ahadi hiyo kama imechelewa sana kwa bara hilo.
"Tumesikitishwa sana na hatua finyu zilizopigwa katika masuala muhimu kwa Afrika," Ali Mohamed, Mwenyekiti wa kundi hilo tawi la Kenya, alisema kwenye mkutano wa COP29.
"Afrika itaendelea kutoa tahadhari juu ya uhaba wa fedha za hali ya hewa."
Akiwahutubia washiriki wa mazungumzo hayo, Simon Stiell, Mkuu wa Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, alikiri kwamba makubaliano hayo yalikuwa hayajatimia kama ilivyotarajiwa.
"Hakuna nchi iliyopata kila walichotaka. Na tunaondoka Baku na mrundikano wa kazi ya kufanya," alisema.
BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED