Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, ametangaza kuachiliwa huru wafungwa kutoka katika magereza mbalimbali nchini humo.
Wale ambao wataachiliwa katika ngazi ya kitaifa ni 5442, sawa na asilimia 41 ya wafungwa 13,211. Kati yao 136 wamefungwa wakiwa na matatizo ya akili.
Aliwapa wanaosimamia utekelezaji wa kifungu hiki muda wa wiki mbili kuwaachilia.
Watakaoachiliwa hasa ni wale waliopatikana na hatia ya makosa madogo, ambao tayari wametumikia kifungo cha miaka minne, wazee na wale wanaosumbuliwa na magonjwa makubwa au ya kudumu.
Operesheni hii iliyofanyika katika jimbo la Muramvya, katikati ya nchi ilifanyika kwa lengo la kupunguza idadi ya wahalifu ambao kwa kawaida hufungwa katika magereza ya Burundi.
Katika hotuba yake, Ndayishimiye alisema: "Kinachotutia wasiwasi sisi sote ni kwamba gharama za matumizi ya juu katika serikali yako mbali na uwezo wake."
“Hapa najua ni wale walioachiwa tu ndio wanalipwa fedha walizokuwa wakizilipa, bila mfungwa huwezi tena kusema wanafunzi wanakosa viti au vitabu. Sikia tunapoteza kiasi gani”.
Rais Ndayishimiye alisema kuwa kila mwaka serikali inatumia takribani faranga bilioni 15 kugharimia shughuli za magereza. Anaona kuwa pesa hizo ni nyingi sana.
Utafiti uliotolewa na shirika la kitaifa la kutetea haki za binadamu la CNIDH mwaka 2023, unaonesha kuwa zaidi ya wafungwa elfu 13 walifungwa katika magereza tofauti nchini Burundi.
BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED